Skip to main content Accessibility help
×
Hostname: page-component-848d4c4894-xfwgj Total loading time: 0 Render date: 2024-06-23T07:34:03.580Z Has data issue: false hasContentIssue false

31 - Kwa Grant Kamenju: Hotuba ya Kuipokea Digrii ya Heshima ya Uzamifu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

from Part V - The Other Ngũgĩ

Published online by Cambridge University Press:  27 July 2019

Ngũgĩ wa Thiong'o
Affiliation:
Distinguished Professor of English and Comparative Literature at the University of California, Irvine.
Get access

Summary

Mwaka 2004 nilialikwa na Chuo Kikuu cha Transkei ambacho sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha Walter Sisulu, Africa Kusini, ili kupokea digrii ya heshima ya uzamifu (au ya udaktari wa falsafa), pamoja na Nelson Mandela na Ali Mazrui. Hafla hiyo ilikuwa pia ni ya kuadhimisha kubadilishwa jina la zamani la Chuo Kikuu hicho, na kupewa jina hilo jipya. Jina lake la zamani, yaani Transkei, lilikuwa na kumbukumbu za utawala wa ubaguzi wa rangi wa kuigawa nchi. Na hilo jina la sasa lina uhusiano na shujaa wa taifa.

Nikiwa pamoja na mke wangu na watoto wawili, tuliwasili kwenye maeneo ya Chuo ambako kulikuwa kumetundikwa mabango yaliyoandikwa HOMECOMING (yaani KURUDI NYUMBANI/ KARIBU NYUMBANI) Niliguswa moyoni: Hiyo ilikuwa ni digrii yangu ya kwanza ya heshima niliyotunukiwa na chuo kikuu cha Afrika, baada ya nyingine kadhaa nilizotunukiwa na vyuo vikuu vya Ulaya na Marekani. Lakini hilo bango la HOMECOMING – ambalo ni jina la kitabu changu kimojawapo – lilikuwa na maana nyingine muhimu. Nilikuwa ninarudi nyumbani Kenya, kwa kupitia Afrika ya Kusini, baada ya kulazimika kuishi uhamishoni kwa miaka ishirini na mbili. Huko kurudi nyumbani kwa kupitia Afrika ya Kusini, kilele chake kilikuwa kiwe Kenya; watoto wangu wawili waliozaliwa uhamishoni walikuwa hawajaigusa ardhi ya Kenya.

Yaliyotokea baada ya siku kumi na moja tangu kurudi nchini kwangu kwa furaha kuu, pamoja na digrii niliyotunukiwa Afrika nikiwa njiani kurudi nyumbani, sasa ni historia. Kurudi kwangu nyumbani kukageuka kuwa ni jinamizi. Mimi na mke wangu tuliponea chupuchupu, baada ya kuvamiwa na watu wanne wenye bunduki/ bastola.

Si makosa ya Afrika ya Kusini, kwamba digrii yangu ya kwanza ya heshima kutoka Afrika pia ina kumbukumbu za ugaidi. Hii ya leo ni digrii ya kwanza ya heshima tangu usiku ule wa ugaidi.

Makamu Mkuu wa Chuo: Mimi ni mwandishi; yaani mimi ni mhunzi wa maneno (au mfua maneno). Lakini nimekosa maneno muwafaka ya kueleza jinsi heshima hii – ambayo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imenipa leo – ilivyo na maana kubwa kwangu. Si kwa sababu tu ya kwamba ni matumaini yangu kuwa nitaweza kuisherehekea digrii hii kutoka Afrika bila ya furaha yangu kufujika; lakini hasa ni kwa sababu ya hadhi ya Chuo Kikuu hiki katika usomi na siasa za Afrika.

Type
Chapter
Information
Ngugi
Reflections on his Life of Writing
, pp. 183 - 185
Publisher: Boydell & Brewer
Print publication year: 2018

Access options

Get access to the full version of this content by using one of the access options below. (Log in options will check for institutional or personal access. Content may require purchase if you do not have access.)

Save book to Kindle

To save this book to your Kindle, first ensure coreplatform@cambridge.org is added to your Approved Personal Document E-mail List under your Personal Document Settings on the Manage Your Content and Devices page of your Amazon account. Then enter the ‘name’ part of your Kindle email address below. Find out more about saving to your Kindle.

Note you can select to save to either the @free.kindle.com or @kindle.com variations. ‘@free.kindle.com’ emails are free but can only be saved to your device when it is connected to wi-fi. ‘@kindle.com’ emails can be delivered even when you are not connected to wi-fi, but note that service fees apply.

Find out more about the Kindle Personal Document Service.

Available formats
×

Save book to Dropbox

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Dropbox.

Available formats
×

Save book to Google Drive

To save content items to your account, please confirm that you agree to abide by our usage policies. If this is the first time you use this feature, you will be asked to authorise Cambridge Core to connect with your account. Find out more about saving content to Google Drive.

Available formats
×